Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka nchini (DPP) imeipa mamlaka Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha, kusikiliza kesi ya uhujumu uchumi inayo mkabili aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya na wenzake.

Ofisi hiyo imewasilisha hati kupitia Wakili wa Serikali Mwandamizi, Tarsila Gervas wakati kesi hiyo ilipofikishwa Mahakamani hapo kwa ajili ya kutajwa.

Sabaya na wenzake wanakabiliwa na mashitaka matano ikiwemo utakatishaji wa fedha na rushwa

Washitakiwa wengine katika kesi hiyo ya uhujumu uchumi namba 27,2021 ni Enock Mnkeni, Watson Mwahomange, John Aweyo, Sylvester Nyegu, Jackson Macha na Nathan Msuya.

Magonjwa ya damu yapatiwa suluhisho Muhimbili
Mkurugenzi Halmashauri ya Gairo asimamishwa kazi