Kesi ya Uhujumu Uchumi inayomkabili aliyekuwa Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Harry Kitilya na wenzake, imeahirishwa hadi Januari 20 mwaka huu kutokana na upelelezi kutokamilika.
Wakili Mwandamizi wa Serikali, Mutalemwa Kishenyi amedai kuwa Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Kisutu, Wilbard Mashauri kuwa kesi hiyo imekuja kwa ajili ya kutajwa na kwamba hakimu anayesikiliza kesi hiyo, Cyprian Mkeha, hayupo.
Aidha Wakili Esterzia Martin, alidai kuwa jalada la kesi hiyo lipo Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), kwa ajili ya kuendelea kuchunguza nyaraka.
Hata hivyo, ameiomba Mahakama ipange tarehe nyingine kwa ajili ya kueleza upelelezi umefikia wapi. Mbali na Kitilya, wengine ni mshindi wa Mashindano ya Urembo (Miss Tanzania) mwaka 1996, Shose Sinare na Mwanasheria wa Benki ya Stanbic, Sioi Solomon. Kwa pamoja, washtakiwa hao wanakabiliwa na mashtaka manane, likiwemo kutakatisha fedha, dola za Marekani milioni sita.

Lissu: Serikali inawajibu wa kumtafuta Saanane
Majaliwa kutuma kamati ya uchunguzi Kampuni ya TANCOAL