Mashauri ya matunzo ya watoto yameelezwa kushika kasi siku hadi siku kutokana na wanawake wengi kuzalishwa na kutelekezwa na watoto wao na wengine kutelekezwa wakiwa wajawazito huku waliowapa wakiwa hawajulikani walipo.

Hayo yamebainishwa na mratibu wa chama cha wanasheria wanawake mkoani Tanga (Tawla) wakili Latifa Mwambondo wakati akizungumza na waandishi wa habari.

Licha ya kutotoa idadi ya mashauri hayo wakili huyo amesema lipo kundi kubwa la wasichana wadogo ambao wameanza kuleta watoto au kujifungua wakiwa na umri mdogo hali ambayo imesababisha hadi ongezeko la watoo wa mitaani.

Mbali na mashauri ya matunzo amesema suala la mirathi nalo limekuwa likiongoza kwa kuwa na mashauri mengi mahakamani kwani kwenye baadhi ya familia kumeibuka uvamizi wa mali za marehemu alizoachiwa mjane na watoto.

Amesema hali hiyo imesababisha ongezeko la migogoro huku wahusika wakishindwa kupeleka mahakamani mrejesho unaofaa hivyo kuwa mateso kwa wanawake wajane.

Mambo 11 mwanaume anayomjaribu mwanamke kama anafaa kuwa mke
Waziri Mkuu apigania malipo kazi za wasanii nchini