Mbunge wa Nkasi Kaskazini kupitia chama ca mapinduzi (CCM), Ally Kessy amelalamikia juu ya uwepo elimu hafifu hususani kwa baadhi ya kinamama, na kueleza imepelekea mama mmoja ambaye alikuwa ni mjamzito jimboni kwake kujifanyia operesheni mwenyewe, kwa kutumia wembe bila kwenda Hospitali.

Ameyasema hayo bungeni jijini Dodoma katika kipindi cha maswali na majibu, ambapo Mbunge Kessy amesema kuwa mama huyo kwa sasa hali yake ni mbaya zaidi, lakini alifanikiwa kujifungua na mtoto wake anaendelea vizuri.

“Vifo vingine vya kinamama vinatokana na kina mama wenyewe, juzi tu jimboni kwangu kuna mama mmoja tena zao lake la nane, kachelewa mwenyewe makusudi kwenda kituo cha afya, kajifanyia operesheni mwenyewe, hii ni hatari sana,”amesema Kessy

Aidha, Kessy amesema kuwa yule mama alimua kujifanyia oparesheni mwenyewe kwa kutumia wembe na kutoa mtoto, sasa hivi yuko Hospitali hali yake si nzuri ila hali ya mtoto ni nzuri, kwa hiyo wakati mwingine vifo vya kina mama vinatokana na wao wenyewe.

Wakuu wa mikoa waonywa kuhusu matamko wanayoyatoa
Habari kubwa katika Magazeti ya Tanzania leo Juni 1, 2019