Mbunge wa Jimbo la Nkasi Kaskazini kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Ali Kessy amesema kuwa kuna baadhi ya viongozi na watoto wa vigogo ambao wamekuwa wakitafuna fedha za miradi ya maji, ambao pia wamekuwa wakimfuata kumuomba asiwataje.

Ameyasema hayo Bungeni Jijini Dodoma wakatika akichangia katika mjadala wa bajeti ya Wizara ya Maji na Umwagiliaji ya mwaka 2018/19 ambapo amesema kuwa mikataba mingi iliyoingiwa ni ya ujanja ujanja.

Amesema kuwa anawajua wote watafunaji wa fedha za miradi ya maji na kwamba wamewahi kumuita na kumuomba anyamaze lakini yeye ameendelea kupiga kelele na kufanikiwa kuokoa bilioni 3 za miradi ya maji.

“Viongozi wakubwa ndio wenye miradi hiyo, na wamekuwa wakinitafuta kuninyamazisha, nikawaambia sipo tayari kunyamaza hata kidogo kwasababu wananchi wanaendelea kutaabika,”amesema Kessy

Zitto amshauri Spika Ndugai
TMA yatabiri ujio wa mvua kubwa kwa siku tano

Comments

comments