Mchekeshaji maarufu wa Marekani, Kevin Hart amefunga ndoa na aliyekuwa mpenzi wake wa siku nyingi, Eniko Parrish jijini California.

Wawili hao wamefikia ndoto zao baada ya kuchumbiana rasmi mwaka 2014 katika siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa ya mrembo huyo.

Tukio hilo lilihudhuriwa na marafiki wachache wa karibu huku watoto wawili wa Kevin Hart ambao sio watoto wa Eniko Parrish.

Kevin Hart alimsifia mkewe huyo akieleza kuwa amemvumilia sana kwenye magumu aliyoyapitia hadi kuwa na shangwe alizonazo hivi sasa. Lakini pia alieleza kuwa alihisi tayari wameshaoana miaka mingi iliyopita kwakuwa walikuwa wanaishi pamoja.

“Nilishajisikia nimeoa, hii ndoa ni kwa ajili yake tu,” alisema Hart.

Sigara Ya Mita 90 Kusherehekea Miaka 90 Ya Fidel Castro Yatengenezwa
Paul Makonda kupanda ulingoni kupigana masumbwi na Cheka