Shirikisho la Soka Korea Kusini limekanusha taarifa za kujiuzulu kwa Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa hilo Paulo Bento, saa chache baada ya kikosi chake kuondolewa kwenye Fainali za Kombe la Dunia zinazoendelea nchini Qatar.

Korea Kusini ilikubali kupoteza mchezo wa Hatua ya 16 Bora mbele ya Brazil kwa kufungwa 4-1 jana Jumatatu (Desemba 05), mchezo ambao uliunguruma kwenye Uwanja wa 974, mjini Doha.

Taarifa iliyotolewa na Shirikisho la Soka la nchi hiyo ya Barani Asia imeeleza kuwa, Kocha huyo kutoka nchini Ureno hajajiuzulu, na badala yake amerejea nyumbani kwao kupumzika na kisha atarudi kuendelea na kazi yake.

“Bento hajajiuzulu, anaenda kupumzika na kufikiria mustakabali wake” imeeleza taarifa hiyo

Taarifa za kujiuzulu kwa Bento ziliibuka baada ya kuzungumza na Vyombo Vya Habari ambapo alinukuliwa akisema: “Ninawashukuru wote kwa yote.”

“Nimekwisha waeleza wachezaji na Rais wa Shirikisho,huu ni uamuzi nilioufanya tangia Septemba, nilishaamua, sasa ninathibitisha. Ninawashukuru wote kwa yote”

Bento mwenye umri wa Miaka 53 amekingoza kikosi cha Korea Kusini tangu mwaka 2018.

Aucho afunguka hatma yake Young Africans
Jeshi, Viongozi wa kiraia wasaini makubaliano