Katibu wa Bunge, Stephen Kagaigai amesema kuwa bado bunge hilo halijapeleka orodha ya majina ya wabunge pamoja na mawaziri ambao wana mahudhurio hafifu kwenye bungeni ikiwa ni siku chache tangu Spika, Job Ndugai kutishia kupeleka orodha ya majina hayo kwenye vyama husika.

Kwa mujibu wa Katibu wa Bunge mara baada ya Spika kutangaza orodha hiyo, kazi inayofuata ni utekelezaji wa maagizo hayo ambapo kwa sasa ofisi ya katibu ipo kwenye mchakato kumalizia kupeleka majina hayo.

Amesema kuwa bado suala hilo linashughulikiwa na yatapelekwa majina hayo yaliyotajwa na Spika bungeni katika sehemu husika ili hatua stahiki iweze kuchukuliwa.

Aidha, kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt. Bashiru Ally,  juu ya hatua ya kutajwa kwa orodha ya mawaziri na wabunge wa chama hicho ambao ni watoro bungeni, amesema suala hilo atalijibu Katibu wa itikadi na uenezi, Humphrey Polepole kwa kuwa liko chini ya idara yake.

Hata hivyo, Novemba 15 Spika wa Bunge, Job Ndugai alifunguka orodha ya wabunge na mawaziri ambao wamekuwa na mahudhurio hafifu ambapo alitajwa Waziri wa Katiba na Sheria, Palamagamba Kabudi, Waziri wa Mambo ya Nje Augustine Mahiga, Waziri wa mazingira, January Makamba, pamoja na Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema.

Serikali CCM haihitaji mabaidiliko- Shaka
Video: Utata Fiesta kuzuiwa Dar, Niko Imara, Lissu awasha moto wa mafao ya wafanyakazi