Klabu ya Udinese Calcio (Udinese) inayoshiriki ligi kuu ya Italia (Serie A), imemfuta kazi meneja Massimo Oddo, baada ya kuchoshwa na mwenendo wa utendaji kazi wake, ambao umesababisha kikosi chao kupoteza michezo 11 mfululizo.

Muda mchache uliopita uongozi wa klabu hiyo, umetangaza kumtimua Oddo, na nafasi yake itajazwa na beki wa zamani wa timu ya taifa ya  Croatia na klabu ya Juventus Igor Tudor.

Uongozi ulianza kumjadili Oddo, mara baada ya mchezo wa mwishoni mwa juma lililopita, ambao ulimalizika kwa Udinese kupoteza dhidi ya Crotone, na kuiacha klabu hiyo ya Dacia Arena ikishika nafasi ya 15 kwenye msimamo wa ligi ya Italia.

Nafasi hiyo inaiweka hatarini Udinese katika sakata la kushuka daraja mwishoni mwa msimu huu, kwani mpaka sasa wana tofauti ya alama nne dhidi ya Benevento wanaoburuza mkia kwa kuwa na alama 17.

“Klabu ya Udinese inatangaza kumfuta kazi Massimo Oddo na nafasi yake itashikwa na Igor Tudor.” Imeeleza taarifa ya klabu hiyo iliyochapishwa kwenye tovuti ya Udinese.

Image result for Igor TudorIgor Tudor

Taarifa hiyo imeendelea kubainisha kuwa, uongozi wa Udinese unafanya mpango wa kumtambulisha rasmi Tudor katika mkutano na waandishi wa habari ambao utafanyika kabla ya mchezo wa mwishoni mwa juma hili.

Tudor ana zuoefu wa kutosha, na tayari ameshazinoa klabu za nchini Uturuki kama Galatasaray na Karabukspor.

Oddo, ambaye ni sehemu ya kikosi cha Italia kilichotwaa ubingwa wa dunia mwaka  2006, alijiunga na klabu ya Udinese kama mkuu wa benchi la ufundi mwezi Novemba mwaka 2017, akichukua nafasi ya Luigi Delneri.

Video: JPM awataka Wabunge wa Afrika Mashariki kudumisha umoja na mshikamano
Ufaransa yampoteza Henri Michel

Comments

comments