Kamishna Mkuu Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Charles Kichere amemsimamisha kazi Meneja wa TRA Mkoa wa Mara, Nicodemus Mwakilembe kutokana na uzembe wa kutosimamia vizuri matumizi ya Mashine za Kielektroniki za kutolea risiti (EFDs) kwa wafanyabiashara.

Kamishana Kichere amesema kuwa meneja huyo ameonesha uzembe wa hali ya juu kwani kuna wafanyabishara wengi mkoani hapo ambao walishalipa fedha kwa ajili ya kupata mashine za EFD lakini hadi sasa hawajapatiwa mashine hizo.

“Wilayani Bunda, kuna wafanyabiashara ambao walikwisha kulipia mashine tangu mwaka 2013, 2014 na 2015 lakini hadi sasa walikuwa bado hawajapatiwa mashine za EFD na wamekuwa wakitumia mwanya huo kama kinga ya kutochukuliwa adhabu na TRA wakati Meneja wa Mkoa yupo na hachukui hatua zozote” amesema Kichere.

Katika ziara ya kushtukiza ya Kamishna Kichere imewezesha wafanyabiashara waliokuwa wamelipia mashine za EFD miaka ya nyuma, kupata mashine hizo na kufundishwa jinsi ya kuzitumia ambapo wengine wamejitokeza kununua mashine hizo kwa ajili ya biashara zao

Ndugulile: Mama wajawazito wanapaswa kupata huduma za matibabu bure
LIVE: Yanayojiri Bungeni Dodoma leo Februari 5, 2018

Comments

comments