Baada ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa mahakama ya Mbeya , Michael Mteite kuwahukumu mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi maarufu kama Sugu na Katibu wa Chadema Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Emmanuel Masonga kifungo cha miaka mitano wakili, Peter Kibatala amesema wanakusudia kukata rufaa.

Kibatala amesema hayo mara baada ya kesi hiyo kumalizika na hukumu ya Sugu na Masonga kutolewa na ameeleza vyombo vya habari kuwa watatoa taarifa kamili  na kueleza nini kinaendelea kuhusu rufaa inayotarajiwa kukatwa.

Joseph Mbilinyi na Emmanuel Masonga wamehukumiwa leo Februari 26, 2018 kwa kudaiwa kutenda kosa la kutumia lugha ya fedheha dhidi ya Rais Dkt. Magufuli wakiwa kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika mnamo Disemba 30, 2017 eneo la uwanja wa shule ya msingi Mwenge mjini Mbeya.

Kufuatia hukumu hiyo baadhi ya wasanii wa muziki wa bongo fleva wamefunguka na wengine wakimtia moyo kuwa gerezani sio kaburini hivyo atamaliza muda wake.

Nikki wa Pili amesema ” Nguvu ya Mungu ikapate kuwa nawe pamoja na familia yako, gerezani sio kaburuni ‘stay strong” Jongwe.

Rama Dee naye amefunguka kuwa ” Nasikitika sana kwa hii habari kama msanii pia kama rafiki wa Sugu amesema hii si picha nzuri”.

Hata hivyo, kwa mara ya kwanza, washtakiwa hao mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi “Sugu” na Katibu wa CHADEMA Kanda ya Nyasa, Emmanuel Masonga walifikishwa Mahakamani Januari 16 na kusomewa mashtaka na Wakili Mkuu wa Serikali, Joseph Pande ambapo kesi yao ilikuwa ikosomwa kwa muendelezo mpaka ilipofikia Februari 09, 2018 ambapo waliachiwa kwa dhamana ya milioni tano kwa kila mmoja.

 

Zitto ataka hesabu ya wapinzani waliobaki
Bondia afariki dunia baada ya kushinda pambano