Pamoja na juhudi zinazofanywa na Serikali za kukomesha mauaji lakini hali inaonekana kuwa bado tete Wilayani Kibiti mkoani Pwani baada ya viongozi wengine wawili kupigwa risasi usiku wa kuamkia leo.

Viongozi waliopigwa risasi ni Mtendaji wa Kijiji cha Mangwi kilichopo katika Kata ya Mchukwi, Shamte Makawa na Mwenyekiti wa Kitongoji cha Mangwi, Maiko Nicholaus.

Aidha, Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Pwani, Onesmo Lyanga amekiri kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa upelelezi unaendelea ili kuwabaini wale waliohusika katika tukio hilo.

Hata hivyo, watu 37 wameuawa tangu vitendo hivyo vianze katika Wilaya za Kibiti, Rufiji na Mkuranga mkoani Pwani wakiwemo askari 13.

Wamarekani waupinga mnara wenye amri 10 za Mungu
Malinzi, Mwesigwa wakamatwa, watuhumiwa kutumia vibaya ofisi