Mshambuliaji Kibu Denis ametwajwa kwa mara ya pili mfululizo kuwania tuzo ya Mchezaji Bora wa Mashabiki wa Klabu ya Simba kwa mwezi Juni, baada ya kuonyesha uwezo mkubwa wa kuisaidia timu yake kwa mwezi huo.

Simba SC imetaja majina matatu ya wachezaji wanaowania tuzo hiyo, na kuwaachia mashabiki kuamua kwa kupiga kura kupitia Tovuti ya klabu, ili kumpata mshindi wa mwezi Juni.

Wachezaji wengine walioingia kwenye Kinyang’anyiro hicho ni Viungo Washambuliaji Pape Osman Sakho (Senegal) na Peter Banda (Malawi), ambao watampa upinzani Kibu Denis anayeshikilia tuzo ya mwezi uliopita.

Wakati huo huo Uongozi wa Simba SC umetoa shukurani kwa Mashabiki wake baada ya kumaliza msimu wa 2021/22, ikiwa nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Uongozi wa Simba SC umetoa shukurani hizo kupitia kurasa za Mitandao ya Kijamii za klabu hiyo, kwa ujumbe ulioandikwa kwa maandishi makubwa ‘AHSANTENI MASHABIKI WETU’.

“Tuna kila sababu ya kuwashukuru ninyi mashabiki wetu.”

“Mmekuwa nguzo imara kwa timu yenu katika nyakati zote za msimu huu 2021/22.”

“Menejimenti ya Simba kwa niaba ya Bodi ya Wakurugenzi tunasema; Asanteni sana mashabiki wetu na tunajivunia kuwa na mashabiki wa aina yenu.”

“Tunawaahidi mazuri zaidi msimu ujao.”

AHSANTENI SANA!

Mikakati uzalishaji wa mbolea yafikia pazuri
Takwimu sahihi walemavu kusaidia utungaji sera