Mshambuliaji wa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Simba SC Kibu Denis ataukosa mchezo wa Mzunguuko wa 13 wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Mtibwa Sugar.

Simba SC itakua ugenini Manungu Complex mkoani Morogoro Jumamosi (Januari 22), ikicheza mchezo huo, baada ya kupoteza dhidi ya Mbeya City kwa kufungwa bao 1-0, Jumatatu (Januari 17) mjini Mbeya.

Taarifa kutoka Simba SC zinaeleza kuwa Kibu hatoweza kucheza mchezo huo, kutokana na majereha ya mguu aliyoyapata kwenye mchezo dhidi ya Mbeya City na kulazimika kutolewa kipindi cha pili.

Naye Kiungo Jonas Mkude hatokua sehemu ya safari ya kuelekea mkoani Morogoro, kufuatia majeraha aliyoyapata kwenye mchezo dhidi ya Mbeya City.

Simba SC pia itaendelea kukosa huduma ya Kiungo kutoka nchini Uganda Taddeo Lwanga, ambaye anatarajiwa kuanza mazoezi mepesi mwishoni mwa mwezi huu.

Polisi Tanzania yaifuata Young Africans Arusha
DJ maarufu Kenya ajiua kwa sumu