Baada ya kuonesha uwezo wa kustaabisha kwa mara ya kwanza akiwa na Taifa Stars dhidi ya Malawi, nyota wa Mbeya City, Kibu Denis amewaingiza vitani mabosi wa Simba na Yanga ambao wameonesha nia ya kutaka saini yake.

Nimepokea simu kutoka pande zote mbili lakini hakuna tulichozungumza zaidi ya kuwataka wafuate taratibu, nadhani hiyo njia sahihi zaidi ya kunipigia simu mara kwa mara,” alisema Kibu na kuongeza:

“Sipendi sana kuzungumzia mambo haya lakini timu yeyote ile naweza kuichezea kikubwa kuwe kuna haki na taratibu zote zimezingatiwa,” alisema.

Hadi sasa Kibu, ndiye anaongoza kwa upachikaji mabao Mbeya City msimu huu akiwa amefunga bao sita licha ya kutocheza kama nusu ya mechi za timu hiyo.

Alijiunga Mbeya City msimu huu akitokea Geita Gold iliyopanda Ligi Kuu msimu huu ambayo ilimsajili kutoka Kumuyange FC ya Ngara iliyokuwa ikishiriki Ligi Daraja la Kwanza (FDL) miaka mitatu iliyopita.

Zitto ataka wachezaji kupewa uraia pacha
Nabi kutema tisa, kusajili wanane