Ile kauli ya kusema wanawake wanaongoza kwa akili kuliko wanaume inazidi kudhiirishwa na wakinamama mbalimbali duniani, ambapo tafiti zinaonesha kuwa wanamke wanauwezo wa kufanya mambo mengi kwa wakati mmoja, ukilinginisha na uwezo huo kwa wanaume na hii imedhihirishwa huko Australia.

Ambapo mwanamke mmoja ambaye ni mbunge, Larissa Waters amevunja rekodi ya kuwa mwanamke wa kwanza duniani kupata ujasiri wa kunyonyesha mtoto bungeni huku akitoa hutuba, kitendo hiki cha pekee kimetokea june 22, mwaka huu bungeni Australia.

Mbunge, Larissa Waters akiwa anatoa hutuba ya madhara ya mapafu yanayowakumba wafanyakazi katika migodi ya kuchumba madini  nchini kwao, huku akimnyonyesha mtoto wake mwenye umri wa siku 14, Alia Joy, ambaye kwa siku hiyo aliweza kuhudhuria bunge kutokana na kazi anayofanya mama yake.

Kitendo alichofanya mbunge Larissa ni kitendo cha kustaajabisha na cha asili kilichowasisimua watu wengi bungeni humo na kuwafanya watabasamu kwa uamuzi aliouchukua mbunge Larissa Waters.

Wachezaji wa kimataifa waweka historia Mlima Kilimanjaro
Ulinzi Mkali Makao Makuu Polisi Wakimsubiri Lowassa