Msemaji wa klabu ya Ruvu Shooting Masau Bwire amesema kikosi cha klabu hiyo hakijapoteza mchezo wa jana Jumapili (Februari 07) dhidi ya Namungo FC sababu ya kuzidiwa uwezo kama ilivyochukuliwa na wadau wengi wa soka la Bongo.

Masau amelipinga hilo kupitia andiko lake alilolichapisha kwenye kurasa za mitandao ya kijamii akeleza kuwa, sababu kubwa ya Ruvu Shooting kupoteza mchezo huo uliochezwa mjini Ruangwa kwenye Uwanja wa Majaliwa ni matokeo ya kizalendo ya kuwapa morari Namungo FC, ambao wanaiwakilisha nchi kimataifa.

“Kwa uwezo wa kuwafunga tuliokuwanao katika mchezo huo, kama tungewafunga, wangepoteza mwelekeo na morari, hivyo huko Angola ingekuwa aibu, tumeepusha aibu hiyo, kwa kuwajenga kisaikolojia na kuwatia moyo kwamba,  wanaweza, wakapambane.”

“Kwa uzalendo wetu, tunawapa majukumu mawili Namungo Fc wakayatende huko Angola, mosi, wakapambane, washinde mechi hiyo, pili, wakaitangaze lugha yetu ya Taifa (Kiswahili), kwa kufanya hivyo, uzalendo tuliowafanyia katika mchezo wa VPL, February 7, 2021, utakuwa wa maana.”

“Uzalendo kwanza. Tuwaunge mkono wote wanaoshiriki mashindano ya Kimataifa,  ambao kwa msimu huu, ni Simba SC na Namungo FC.”

Ameandika MAsau  Bwire. Kupoteza kwa mabao 2-1 dhidi ya Namungo FC, kumeifanya klabu ya Ruvu Shooting kubaki na alama 28 zinaiwaweka kwenye nafasi ya tano katika msimamo wa Ligi Kuu, huku wenyeji wao wakichupa hadi nafasi ya 12 kwa kufikisha alama 21.

Spika Ndugai ''Gambo nafasi bado unayo''
Kaze atuma salamu Mbeya City