Kiungo mshambuliaji wa Simba SC, Shiza Ramadhan Kichuya, ameanza mazoezi na timu yake baada ya kupata nafuu ya majeraha ya kifundo cha mguu aliyoyapata wakati wa mchezo wa mzunguuko wane wa ligi kuu juma lililopita dhidi ya Mbao FC.

Mchezaji huyo aliumia katika dakika ya 44 ya mchezo huo, uliomalizika kwa sare ya mabao mawili kw amawili kwenye Uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza.

Kichuya alifunga bao la kwanza dhidi ya Mbao dakika ya 16 kwa kichwa lakini hata hivyo alishindwa kumaliza kipindi cha kwanza baada ya kupata majeraha kabla ya nafasi yake kuchukuliwa na Haruna Niyonzima.

Kufuatia hali hiyo Kichuya, alikosa mchezo wa kirafiki dhidi ya Milambo FC, juzi kwenye Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora, timu hizo zikitoka sare ya 0-0.

Jana na leo, Kichuya amefanya mazoezi chini ya usimamizi wa daktari wa timu hiyo, Yassin Gembe kwenye Uwanja wa Alliance mjini Mwanza.

Kichuya aliyefunga mabao 12 msimu uliopita akitokea Mtibwa Sugar ya Morogoro, ameshaweka kimiani mabao mawili mpaka sasa kwenye Ligi Kuu ya Vodacom

Simba imerejea Mwanza ikitokea Tabora ambapo imeweka kambi ya kujiandaa na mchezo wake ujao wa Ligi Kuu dhidi Stand United United.

Mchezo huo utachewa siku ya Jumapili kwenye Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga.

Saudi Arabia yaruhusu wanawake kuendesha magari
Safaricom yajibu tuhuma za kushiriki uchakachuaji matokeo Kenya