Wakulima na wauzaji wa mbogamboga katika masoko ya jiji la Mwanza wamekumbwa na taharuki kufuatia madai ya kuwepo kwa kidudu mtu kinachosemekana kushambulia majani ya kisamvu na kabechi, jambo ambalo linasababisha walaji wa mboga hizo kuhofia usalama wa afya zao.

Baadhi ya wakulima wa mchicha wanalazimika kung’oa mashina yake ili kutengeneza chakula cha kuku kutokana na hofu hiyo.

Kati ya Juni 16 na Julai 3 mwaka huu uvumi kuhusu kidudu mtu kuonekana kwenye mboga za majani, uliibuka baada ya wafanyabiashara wawili wa mboga za majani mmoja kutoka Kisesa na mwingine Kishili kumpeleka mdudu huyo kwa afisa afya wa halmashauri ya jiji la Mwanza ambapo baada ya saa mbili alibadilika na kuwa kipepeo.

Tahadhari ya kiafya inazidi kutolewa kwa wananchi, ingawa hadi sasa hakuna uthibitisho uliotolewa na wataalam juu ya kuwepo kwa kidudu mtu hicho lakini.

Nahodha Wa China Afungiwa Kucheza Soka
Watoto 8 waliofichwa warejeshwa kwa wazazi wao Sumbawanga