Kiungo kutoka DR Congo na klabu ya DC Motema Pembe, Karim Kiekie anatajwa kuwa kwenye mipango ya Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Simba SC, kwa ajili ya michuano ya klabu bingwa Barani Afrika.

Kiekie ambaye kwa sasa yupo nchini Cameroon akiwa sehemu ya timu ya taifa ya DR Congo ambayo juzi ilianza vyema kwenye michuano ya Mataifa Bingwa Barani Afrika ‘CHAN’ anatajwa kuwa miongoni mwa vijana wanaofanya vyema ndani ya uwanja kwa uwezo wake wa kutumia mguu wa kushoto.

Taarifa zinaeleza kuwa kiungo huyo, huenda akajiunga na Simba SC mara baada ya fainali za ‘CHAN’ na usajili wake utaegemea kwenye Michuano ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika pekee.

Mbali na Kikekike Simba SC inatajwa kuwa kwenye mkakati wa kuwasajili wachezaji wengine kwa ajili ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika, ambayo wamedhamiria kufanya vizuri zaidi ya msimu wa 2018/19, ambapo walifuka hatua ya Robo fainali.

Mchezaji kutoka Zimbabwe Peter Mudawa ambaye anacheza ndani ya Klabu ya Highlanders, ni miongoni mwa wachezaji wanaotajwa kuwa mbioni kutua Msimbazi, sanjari na mshambuliaji kutoka Nigeria Junior Lukosa.

Mbali na nyota hao watatu pia kiungo mwingine ambaye anatajwa kuwa kwenye mipango ya Simba SC ni pamoja na Nomore Chinyerere ambaye ni kiraka ndani ya kikosi cha FC Platinum, ambapo alikuwa anakipiga na kiungo mwenzake Chikwende aliesajiliwa mwishoni mwa juma lililopita.

Simba SC imepangwa kundi A na mabingwa watetezi Al Ahly ya Misri, As Vita ya DR Congo pamoja na Al Merrikh ya Sudan.

CHAN 2021: Taifa Stars shughulini leo
Habari kubwa kwenye magazeti leo, Januari 19, 2021