Shirikisho la soka barani Ulaya UEFA limetangaza mchezo wa fainali wa ligi ya mabingwa kwa mwaka 2018 utachezwa mjini Kiev (mji mkuu wa nchi ya Ukraine).

Mjumbe wa kamati kuu ya UEFA Frantisek Laurinec amesema mchezo wa fainali utachezwa kwenye uwanja wa Olimpiki (Olympic Stadium) uliopo mjini humo, wenye uwezo wa kuchukua mashabiki 68,000 walioketi.

Nchi ya Ukraine imepewa heshima hiyo kubwa na huenda mashabiki wa soka nchini humo wakafarijika kwani mwezi mmoja badaae nchi jirani ya Urusi itakua mwenyeji wa fainali za kombe la dunia za mwaka 2018.

UEFA walizitenganisha nchi hizo na kuzitambua kama nchi wanachama (Urusi na Ukraine) kupitia timu zao za taifa na klabu kuanzia Julai 2014.

Tayari kwa mwaka huu UEFA wameshauchagua uwanja wa Principality uliopo mjini Cardiff nchini Wales kuwa mwenyeji wa fainali ya mwaka 2017, ambayo michezo yake ya hatua ya makundi ilianza siku mbili zilizopita.

Wakati huo huo mji mkuu wa Estonia (Tallinn) nao umeteuliwa kuwa mwenyeji wa mchezao wa UEFA Super Cup kwa mwaka 2018 kupitia uwanja wa Lillekula Arena.

Mchezo huo umepangwa kuchezwa Agosti 18, 2018, huku mchezo wa fainali wa michuano ya Europa League kwa mwaka huo ukitarajia kupangiwa tarehe na mji husika siku za usoni.

Katika hatua nyingine kamati kuu ya UEFA imemthibitisha na kumteua Theodore Theodiridis kuwa katibu mkuu wa kudumu ikiwa ni siku moja baada Aleksander Ceferin kuchaguliwa kuwa rais wa shirikisho hilo.

Antonio Conte Kumkabidhi Gwanda David Luiz
Malori kumi na mbili kutoka Tanzania Yatekwa nchini Congo DRC, Manane ni mali ya Mfanyabiashara Azim Dewji