Kiungo kutoka nchini Uganda Tayo Odongo Matthew amejiunga na klabu ya Biashara United Mara inayojiandaa kushiriki Kombe la Shirikisho ‘CAF’.

Odongo mwenye umri wa miaka 24, amejiunga na klabu jiyo ya mkoani Mara kwa mkataba wa miaka miwili akitokea klabu ya Zoo Kericho FC ya Kenya.

Usajjli wa kiungo huyo ni sehemu ya kujiimarisha kuelekea Msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara na Michuano ya Kimataifa (Kombe la Shirikisho Barani Afrika ‘CAF’).

Odongo anaungana na Atupele Green aliesajiliwa na Biashara United usiku wa kuamkia leo, wakitanguliwa na Elias Maguli aliyekuwa FC Platnums ya Zimbabwe.

Biashara United Mara iliyomaliza nafasi ya nne katika msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa 2020/21, itashiriki kwa mara ya kwanza michuano ya kimataifa msimu wa 2021/22.

Rais Samia kwa akina Mbowe: Nataka tukutane, niwaeleze…
Rais Samia afunguka kesi ya Mbowe, ‘ni ugaidi na uhujumu uchumi’