Mara baada ya kupoteza wake wa Ligi kuu Tanzania Bara kwa bao 1-0 dhidi ya Majimaji, Mtibwa Sugar wametoa sababu za kupoteza mchezo huo kupitia kwa afisa habari wake Thobius Kifaru ‘Ligalambwike’.Kifaru amesema kuwakosa nyota wao watatu kwenye mchezo huo uliochezwa mjini Songea, ndio sababu iliyowapelekea kuzikosa pointi tatu.

Wachezaji waliotajwa kukosekana katika mchezo huo ni Andrew Vincent, beki wa kulia wa timu hiyo Issa Rashid ‘Baba Ubaya’ na beki wa kati Salim Mbonde.

“Majimaji wameweza kupata goli moja, goli lililokuwa zuri kwelikweli. Tumecheza vizuri ila kuwakosa nyota wetu Andrew Vincent, Baba Ubaya na Salim Mbonde imekuwa sababu ya kupoteza mchezo wetu wa leo” alisema Kifaru kuliambia Anga la Michezo.

“Mara baada ya kumalizika kwa pambajo letu la leo, mashabiki wa Majimaji walikuwa hawaamini kama timu yao iliibuka na ushindi”.

Katika hatua nyingine Thobius Kifaru hakusita kuwamwagia pongezi waamuzi waliochezesha mchezo wao huo.

“Waamuzi walichezesha vizuri sana, dada zangu hawa, nadhani TFF iangalie namna ya kuwatunza watu kama hawa” aliongeza Kifaru.

Yanga Kuwavaa Maafande Wa JKT Mlale Jumatano
AY afunguka baada ya TCRA kuifungia video ya ‘Zigo Remix’, TCRA nao wanena