Polisi nchini Nigeria imesema inawashikilia Wafanyakazi wa Mwanamuziki kutoka nchini Nigeria Davido kwa ajili ya kuwafanyia mahojiano juu ya kifo cha mtoto wa msanii huyo ambacho kina utata.

Hata hivyo, ripoti za awali zilidokeza kwamba mtoto wa kwanza wa kiume wa Davido alizama kwenye bwawa la kuogelea (swiming pool) iliyopo kwenye makazi yake katika eneo la Kisiwa cha Banana huko Lagos nchini Nigeria.

Katika harakati za kumpatia huduma ya kwanza mtoto huyo mwenye umri wa miaka mitatu, baada ya kutolewa nje ya bwawa la kuogelea, inasemekana alikimbizwa hospitali katika eneo la Lekki jimboni humo ambapo alithibitishwa kufariki na mmoja wa madaktari waliokuwa zamu. .

Hata hivyo, tangu habari za kifo cha Ifeanyi kuenea kwa umma, Wanigeria, hasa wapenzi wa burudani, walionyesha kusikitishwa sana tukio hilo huku wengine wakidhihirisha kukasirishwa na mazingira yanayodaiwa tukio hilo limetokea.

Sheria hewa ya ukaa yaanza kutumika rasmi
Mengi yaibuka kifo cha Msanii Takeoff