Katibu wa Baraza la Michezo Taifa (BMT) Mohammed Kiganja amesema Elimu aliyoipata ya stashahada ya juu ya mambo ya mahusiano ya kimataifa, ataitumia vyema kuweza kutatua migogoro inayoendelea na kuibuka katikavyama mbalimbali vya Michezo pamoja na klabu, ili kuhakikisha michezo inaendelea kustahimili hapa Nchini.

Katibu kiganja ameyasema hayo leo hii tarehe 19 Januari 2018, mara baada ya kutunukiwa Stashahada hiyo ya juu ya mambo ya mahusiano ya kimataifa na aliyekuwa mgenirasmi BALOZI OMBENI SEFUE katika mahafali hayo yaliyofanyika katika chuo kikuu cha diplomasia jijini Dar es salaam.

Aidha katibu Kiganja amesema ifike wakati sasa vilabu vikubwa nchini kama vile Simba na Yanga vinapokuwa na migogoro vianzie katika ngazi ya wilaya kwa maana ya chama cha mpira wa miguu ILALA, ikishindikana kwenda katika chama cha mpira wa miguu cha mkoa na ikishindikana kabisa ndipo baraza linaweza kuingilia kati kupata suluhu.

 

Chadema wamtaja mgombea Kinondoni
Simba SC yamtambulisha rasmi Pierre Lechantre