Aliyekuwa Mkurugenzi wa Mipango, Ufuatiliaji na Tathmini katika Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Kulthum Mansoor amekamatwa saa chache baada ya kutajwa na Rais John Magufuli.

Kigogo huyo anatuhumiwa kuwatapeli wafanyakazi wenzake jumla ya Shilingi bilioni moja, akiwaahidi kuwa atawapa viwanja eneo la Bagamoyo bila kutimiza ahadi yake.

Naibu Mkurugenzi wa Takukuru, Brigedia Jenerali John Mbungo ameeleza kuwa wakati Rais Magufuli anamzungumzia, tayari uchunguzi wa tuhuma dhidi yake ulikuwa umeanza hivyo alikamatwa jana na kulala mahabusu, leo atafikishwa mahakamani.

“Wakati Rais anamzungumzia jana uchunguzi ulikuwa umeanza na alikamatwa na kulala mahabusu katika kituo cha Oysterbay jijini Dar es Salaam, leo [Marchi 29] atafikishwa mahakamani,” Mwananchi wanamkariri Jenerali Mbungo.

Rais Magufuli aliibua sakata hilo alipokuwa akimuapisha Balozi wa Tanzania nchini Cuba, Valentino Mlowola na kupokea ripoti ya Takukuru.

Alisema anashangaa kuona mkurugenzi huyo hachukuliwi hatua yoyote wakati analalamikiwa na wafanyakazi wenzake ambao wanaogopa kumwambia kwa kuwa ni Bosi.

Video: NASSARI kulipa FIDIA Bunge baada ya kushindwa Mahakamani? | "Spika ametekeleza maagizo..."
Kigogo wa Takukuru kuburuzwa mahakamani

Comments

comments