Aliyekuwa Mkurugenzi wa Mipango, Ufuatiliaji na Tathmini wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Kulthum Mansoor anayetuhumiwa kuwadhulumu viwanja wafanyakazi wa taasisi hiyo, amekamatwa na polisi.

Kulthum amekamatwa jana Alhamisi Machi 28, 2019 na kupelekwa kituo cha polisi cha Oysterbay, jijini Dar es Salaam.

Hayo yamethibitishwa na Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Brigedia Jenerali John Mbungo ambapo amesema kuwa ni kweli mtuhumiwa huyo alikamatwa jana na kupelekwa kituo cha polisi Osterbay,

“Ni kweli amekamatwa jana na yuko Oysterbay na leo atafikishwa mahakamani.”amesema Brigadia Jenerali John Mbungo

Aidha, amesema wakati jana Rais Dkt. John Magufuli anamzungumzia kigogo huyo, uchunguzi wa tuhuma zinazomkabili ulikuwa umefikia mwisho, hivyo alikamatwa na kulala mahabusu na leo atafikishwa mahakamani

Hata hivyo, jana, Rais Magufuli akizungumza Ikulu mara baada ya kumuapisha Balozi wa Tanzania nchini Cuba, Valentino Mlowola pamoja na kupokea ripoti ya Takukuru alisema anashangazwa kwa taasisi hiyo kutomchukulia hatua.

Kigogo wa Takukuru aliyetajwa na JPM alala mahabusu
Serikali kusomesha wataalam 100 wa Kilimo nchini Israel