Mlinda mlango chaguo la kwanza kwenye kikosi cha Azam FC Mathias Kigonya ameitwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Uganda ‘The Cranes’.

Kigonya ameitwa kwenye kikosi cha ‘The Cranes’ kwa ajili ya michezo ya kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika ‘AFCON 2022’ dhidi ya Burkina Faso na Malawi itakayochezwa baadae mwezi huu.

Hii ni mara ya kwanza mlinda mlango huyo aliejiunga na Azam FC wakati wa dirisha dogo la usajili, kuitwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Uganda.

Hata hivyo tangu alipojiunga na Azam FC, Kigonya ameonesha kiwango kizuri na kuisaidia klabu yake kuendelea kupambana ili kufikia lengo la kumaliza kwenye nafasi za juu katika Mshike Mshike wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu 2020/21.

Kigonya alijiunga na Azam FC akitokea Forest Rangers F.C ya Zambia, akchukua nafasi ya aliyekua kipa chaguo la kwanza klabuni hapo David Mapigano Kisu, ambaye alionyesha kiwango duni kabla ya kufunguliwa kwa dirisha dogo la usajili mwishoni mwa mwaka 2020.

31 waitwa The Cranes
Hersi Said: Kaze haondoki Young Africans