Mlinda mlango kutoka nchini Uganda Mathias Kigonya, ameizungumzia penati alioiokoa kwenye mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Simba SC jana Jumapili (Februari 07), Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es salaam.

Kigonya alieonekana kuwa mtetezi mahiri kwenye lango la Azam FC amesema kiungo wa Simba SC Clatous Chama alipiga penati ya kawaida jambo ambalo lilimfanya aweze kwenda nayo sawa na kuliweka lango lake salama.

“Ilikuwa ni penati ya kawaida na jukumu langu mimi ni kuweka lango salama kwa ajili ya timu pamoja na kufikia malengo yangu ambayo nimejiwekea.”

“Kupata alama moja ugenini kwetu sio jambo baya hivyo tutajipanga kwa ajili ya michezo yetu ijayo.” Amesema Kigonya

Chama alikosa penati dakika ya 38 iliyosababishwa na Luis Miquissone ambaye alichezewa faulo kwenye eneo la hatari.

Kiungo huyo kutoka nchini Zambia mwenye mabao sita alipiga penati hiyo iliyookolewa na Kigonya hata aliporejea mara ya pili kupiga wachezaji wa Azam FC waliokoa hatari hiyo jambo lililofanya nyota huyo acheze kinyonge dakika zote 45 za kipindi cha pili.

Mchezo huo ulimalizika kwa Azam FC kulazimishwa sare ya mabao 2-2 ambayo inafanya kufikisha jumla ya alama 33 huku Simba SC ikiwa nafasi ya pili na pointi zake ni 39 huku kinara akiendelea kuwa Young Africans kwa kumiliki alama 44.

Kaze: Sipangiwi kikosi
Ugonjwa usiojulikana wamponza Daktari wa Chunya