Uongozi wa klabu ya Simba SC umemfungia kwa mwezi mmoja beki wake, anayeweza kucheza nafasi za kiungo pia, Abdi Banda.

Simba wamemfungia Banda tangu Aprili mosi na maana yake atakuwa huru kurejea kikosini mwishoni mwa mwezi huu.

Pamoja na barua ya kufungiwa kwa Banda kunaswa, lakini bado Siimba imeendelea kufaya siri.

Ofisa Habari wa Simba, Hajji Sunday Manara alisema suala la Banda litatolewa ufafanuzi ili mchezaji huyo aweze kujua hatima Jumatano.

“Kesho (Jumatano) tunakwenda kutoa uamuzi wa suala la Banda, tumekaa na kujadili utetezi wake, sasa tunatoa hukumu,”alisema Manara.

Banda alimgomea kocha Mganda, Jackson Mayanja kuingia dakika ya tano katika mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya Coastal Union, kuchukua nafasi ya Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, akidai ni mapema mno kumtoa beki mwenzake kwa sababu ya makosa machache aliyofanya.

Baada ya mchezo huo ambao Simba ilishinda mabao 2-0, uongozi wa Simba alimtaka Banda kumuomba msamaha kocha Mayanja, lakini akagoma na tangu hapo hakuripoti mazoezini.

Baadaye Banda akatakiwa kuandika barua ya kujieleza kwa nini asichukuliwe hatua kwa utovu wa nidhamu aliofanya, naye akafanya hivyo, ingawa Simba SC wamechukua muda mrefu kutoa uamuzi.

BARUA YA BANDA BARUA YA BANDA1

Kamati Ya Nidhamu Ya TFF Kukutana Mei Mosi
TFF Yamtangaza Afisa Habari Mpya