Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla ametoa ya moyoni akieleza kuwa mahasimu wake aliodai walipanga kumuua; wanafanya njama za kumchafua aondolewe kwenye nafasi ya uwaziri.

Akieleza kupitia ukurasa wake wa Instagram, Waziri Kigwangalla ambaye hakuwataja ‘mahasimu’ wake, akieleza kuwa wanamhasimu kwakuwa wana ‘dili’ lao ambalo amelikwamisha kwakuwa ni lazima liidhinishwe na waziri. Kwa mujibu wa Waziri Kigwangalla, watu hao wanataka kula fedha za Serikali hivyo ameeleza kuwa atakutana nao mahakamani.

Amesema watu hao wamekuwa wakimfuatilia kwa lengo la kumtoa uhai wake, na kwamba hata alipolazwa ‘ICU’ katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili baada ya kupata ajali ya gari aliwekewa ulinzi mkali na Serikali; na baadaye aliambiwa kuna tishio dhidi yake.

Desemba mwaka jana, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli aliwaonya Waziri Kigwangalla na Katibu Mkuu wake, Profesa Adolf Mkenda akiwapa siku tano kutatua mgogoro kati yao vinginevyo atatengua uteuzi wao.

Hivi ndivyo alivyoandika: 

Sikusudii kufanya press conference. Watu wengi wamenishauri niishie hapa. Team yangu imefanya kazi nzuri, imenipa uthibitisho wa majina ya wanaotaka nichafuliwe ili niondolewe uwaziri. Bahati mbaya hakuna cha kunichafua nacho, wanapika hadithi za kitoto na kurudia tu. Walidhani ningekaidi maelekezo ya Mhe. Rais juu ya mgogoro wa ndani ya Wizara yetu ili Rais achukie aniondoe, wakakwama. Sikukaidi. Wakaona wafanye mwendelezo kupitia gazeti, sijataka kujibishana nalo, tutakutana mahakamani ambapo mbivu na mbichi zitajulikana, ukweli utawekwa wazi na rekodi itakaa sawa. Sijashangaa kuwa wahusika ni wale wale wa kipindi kilichopita.

Hakuna jipya. Sababu ni deal yao binafsi, ambayo haitekelezeki bila ridhaa ya Waziri, na bahati mbaya kwao Waziri ni mimi; walitamani nisiwepo watafune pesa za serikali vizuri, wamekwama. Tutaendelea kudhibiti kimya kimya. Kwa wanaokumbuka wakati nimelazwa ICU na baadaye wodini, ilikuwa ngumu sana kunitembelea na kuniona. Paliwekwa ulinzi mkali sana na watu wote walizuiliwa kuingia isipokuwa kwa kibali cha Ikulu, hadi Mawaziri wenzangu hawakuruhusiwa.

Nilishangaa sana lakini niliambiwa ndiyo hivyo. Baadaye nikaja kujua kuwa kuna watu walipanga njama za kuniua na hiyo ingeweza kuwa fursa kwao kunimalizia. Baada ya kuteuliwa tu Wizara hii kulizuka mtafaruku mkubwa sana juu ya usalama wangu, nilifuatiliwa kila kona mpaka serikali ikanipa walinzi, nilibisha kwa kuwa sipendi attention sana lakini nililazimishwa na kuambiwa nipo kwenye ‘threat’! Sikuwa na option. Nilianza kuishi kwa hofu na mashaka sana.

Hivyo, baada ya ajali na yaliyotokea kutokea nililazimika kuwa makini zaidi. Imani yangu kwa kila mtu ilipungua. Nikawa ‘alert’ wakati wote. November 2019 nililetewa taarifa za kutisha, nikaongeza umakini. Team yangu imenisihi nisiweke majina hadharani na kwamba wanawafuatilia wahusika kwa ukaribu na watazijulisha mamlaka kwa hatua stahiki zaidi. Watu wa karibu sana na mimi nimewapa mpango na taarifa zote na wanajua cha kufanya endapo chochote kitanitokea. Kuna mbinu nyingi za mapambano. Tuendelee tu! #HK

 

View this post on Instagram

 

Sikusudii kufanya press conference. Watu wengi wamenishauri niishie hapa. Team yangu imefanya kazi nzuri, imenipa uthibitisho wa majina ya wanaotaka nichafuliwe ili niondolewe uwaziri. Bahati mbaya hakuna cha kunichafua nacho, wanapika hadithi za kitoto na kurudia tu. Walidhani ningekaidi maelekezo ya Mhe. Rais juu ya mgogoro wa ndani ya Wizara yetu ili Rais achukie aniondoe, wakakwama. Sikukaidi. Wakaona wafanye mwendelezo kupitia gazeti, sijataka kujibishana nalo, tutakutana mahakamani ambapo mbivu na mbichi zitajulikana, ukweli utawekwa wazi na rekodi itakaa sawa. Sijashangaa kuwa wahusika ni wale wale wa kipindi kilichopita. Hakuna jipya. Sababu ni deal yao binafsi, ambayo haitekelezeki bila ridhaa ya Waziri, na bahati mbaya kwao Waziri ni mimi; walitamani nisiwepo watafune pesa za serikali vizuri, wamekwama. Tutaendelea kudhibiti kimya kimya. Kwa wanaokumbuka wakati nimelazwa ICU na baadaye wodini, ilikuwa ngumu sana kunitembelea na kuniona. Paliwekwa ulinzi mkali sana na watu wote walizuiliwa kuingia isipokuwa kwa kibali cha Ikulu, hadi Mawaziri wenzangu hawakuruhusiwa. Nilishangaa sana lakini niliambiwa ndiyo hivyo. Baadaye nikaja kujua kuwa kuna watu walipanga njama za kuniua na hiyo ingeweza kuwa fursa kwao kunimalizia. Baada ya kuteuliwa tu Wizara hii kulizuka mtafaruku mkubwa sana juu ya usalama wangu, nilifuatiliwa kila kona mpaka serikali ikanipa walinzi, nilibisha kwa kuwa sipendi attention sana lakini nililazimishwa na kuambiwa nipo kwenye ‘threat’! Sikuwa na option. Nilianza kuishi kwa hofu na mashaka sana. Hivyo, baada ya ajali na yaliyotokea kutokea nililazimika kuwa makini zaidi. Imani yangu kwa kila mtu ilipungua. Nikawa ‘alert’ wakati wote. November 2019 nililetewa taarifa za kutisha, nikaongeza umakini. Team yangu imenisihi nisiweke majina hadharani na kwamba wanawafuatilia wahusika kwa ukaribu na watazijulisha mamlaka kwa hatua stahiki zaidi. Watu wa karibu sana na mimi nimewapa mpango na taarifa zote na wanajua cha kufanya endapo chochote kitanitokea. Kuna mbinu nyingi za mapambano. Tuendelee tu! #HK

A post shared by Dr. Hamisi Kigwangalla (@hamisi_kigwangalla) on

Idadi wasioajiriwa yaongezeka lukuki, vijana wafikia milioni 267
NEMC yanasa mifuko feki Njombe