Serikali kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii, imetengeneza filamu maalum kwaajili ya kutangaza utalii wa Tanzania kwa lugha mabalimbali duniani.

Waziri wa Maliasili na utalii Dkt. Hamis Kigwangalla amewaomba watanzania kusambaza mitandaoni na kwa njia nyingine filamu hiyo ya utalii ili kuwafikia watu wengi ulimwenguni.

Kigwangalla amesema hayo wakati akizindua filamu hiyo jijini Dar es salaam huku akiwahakikishia watalii kuwa tahadhari zote zimewekwa kwa kuwakinga na maambukizi ya virusi vya Corona.

Devota Mdachi Murugenzi mwendeshaji Bodi ya Utalii Tanzania amesema filamu hiyo imetafsiriwa kwa lugha mbalimbali ili kuwafikia watalii wengi zaidi.

Ikumbukwe kuwa hivi karibuni Rais John Magufuli alitangaza kufunguliwa kwa huduma za utalii hapa nchini baada ya kufungwa kwa muda kutokana na janga la Corona.

UN yamulika mauaji ya mtu mweusi Marekani
Aua mtoto wa siku mbili baada ya kutelekezwa na mwanaume