Kwenye kila changamoto kuna fursa. Hicho ndicho kilichomtokea Zuwena ‘Shilole’ Muhamed ambaye ametumia changamoto ya kuhangaika na kiingereza kibovu kuwa fursa ya kufanikisha adhma yake.

Shilole ambaye amekuwa akivunja mitandao ya kijamii kwa kuzungumza kiingereza cha kuungaunga, akikosea maneno na sentensi bila kujali, amepewa nafasi ya kufundishwa kuzungumza kiingereza fasaha na Kituo cha Utamaduni cha Uingereza (British Council), pamoja na mkataba wa kazi mwaka mmoja.

Mwimbaji huyo wa ‘Mchakamchaka’ amesema kuwa baada ya kuona kipande cha video kinachomuonesha akihangaika kutamka neno ‘subscribe’ na mengine, alipigiwa simu moja kwa moja na Uongozi wa British Council na kupewa nafasi hiyo ambayo aliichangamkia bila kusita.

Pamoja na kupewa fursa hiyo, Shilole pia amepewa nafasi ya kufanya kazi kwenye kituo hicho kwa muda wa mwaka mmoja punde atakapohitimu masomo hayo yatakayochukua miezi mitatu tu.

“Nikimaliza kusoma nitapewa mkataba wa kufanya nao kazi kwa mwaka mzima. Ninasoma bure, darasa nililopo lina wanafunzi 15. Nimefurahi sana kwakweli kupata fursa hii,” Mwananchi limemkariri Shilole.

Shilole akiwa na uongozi wa British Council

British Council ina wataalam wa kiwango cha kimataifa wanaofundisha lugha ya kiingereza kwa muda mfupi.

Hongera kwa ShiShi kwa kupata fursa hiyo, tunatumaini baada ya miezi mitatu mahangaiko ya Kiingereza yatakuwa historia kwake.

Pata picha Shilole anatiririka ‘kizungu’ kama Vee Money! Kwa msemo maarufu wa Kiswahili kisicho rassmi, ‘Utamtaka’.

Israel yatungua ndege ya kivita ya washirika wa Urusi
Jafo ‘kula sahani moja’ na wanafunzi wanaotumia simu shuleni

Comments

comments