Kijana mwenye umri wa miaka 18 aliyedukua mifumo ya mawasiliano ya Shirika la Upelelezi la Marekani (FBI) pamoja na Shirika la Ujasusi la Marekani (CIA) akiwa chumbani kwake, amehukumiwa kifungo cha miaka miwili.

Jaji ustice Haddon-Cave amemhukumu kifungo hicho atakachokitumikia ndani ya ‘jela ya watoto watukutu’ baada ya kumkuta na hatia ya kudukua taarifa za siri za vitengo hivyo muhimu vya usalama wa Marekani.

Kane Gamble anadaiwa kufanya ugaidi wa kimtandao kwa kulenga kupata taarifa za Marekani kuhusu Afghanistan na Iraq, kitendo ambacho kimeelezwa kuwa kiliathiri ufanisi wa mifumo ya mashirika hayo.

Akijitetea mahakamani hapo, Gamble aliyekiri mashtaka dhidi yake alisema kuwa hakuwa na nia yoyote ya kuleta madhara bali alikuwa akifanya udukuzi huo kama sehemu ya kujifurahisha tu, utetezi ambao ulitupiliwa mbali.

Jaji Haddon-Cave alisisitiza kuwa Gamble alitumia taarifa hizo kama sehemu ya kampeni yake ya ugaidi wa kimtandao.

Anadaiwa kufanya makosa hayo kati ya Juni 2015 na Februari 2016 akiwalenga aliyekuwa mkuu wa CIA, John Brennan na Mkurugenzi Msaidizi wa FBI, Mark Giuliano kutoka nyumbani kwake eneo la Linford Crescent, Coalville.

Magazeti ya ndani na nje ya Tanzania leo Aprili 21, 2018
Democratic wamburuza mahakamani Trump na timu yake