Kijana aliyetambulika kwa jina la Ajun (21), raia wa nchini China, aliyezaliwa na vidole 9 kwenye mguu wake wa kushoto amefanyiwa upasuaji na kubaki na vidole 5 kama watu wengine.

Kabla ya kufanyiwa upasuaji huo alikumbana na pingamizi kutoka kwa wazazi wake waliokuwa na imani potofu ambao hawakutaka afanyiwe upasuaji walitaka abaki hivyohivyo maisha yake yote.

Amesema maisha yake yote ya utotoni alikuwa anaishi kwa kujitenga kuepuka unyanyapaa, alipofika darasa la tatu aliacha kabisa kuvaa viatu vya wazi kuepuka maneno ya watu.

Wazazi wake waliamini kuzaliwa hivyo ni mkosi jambo ambalo na yeye ilimbidi aamini, hajawahi kuwa na mpenzi kwani alijiona hajakamilika kama watu wengine hivyo hakuna msichana ambaye angekubali kuwa nae katika mapenzi.

Ameeleza kuwa baada ya wazazi wake kutojali hali yake, aliamua kujiwekea nadhiri kwamba akiwa mkubwa atajishughulikia mwenyewe kwenda kufanyiwa upasuaji, amefurahi kuona sasa nadhiri yake imetimia.

Upasuaji wake ulichukua masaa tisa na jopo la madaktari waliongozwa na daktari Wu Xiang ambaye amesema ni nadra sana kuona mtu amekaa miaka yote hiyo na tatizo hilo bila kufanyiwa upasuaji.

T.I.D amaliza bifu na mtu aliyegombana naye
Simba yadaiwa kumnyatia kiungo wa Zesco

Comments

comments