Kituo cha sheria na haki za binadamu LHRC kimewataka viongozi wa serikali na viongozi wa vyama vya siasa kuacha kutoa matamko ya kichochezi badala yake wajenge utamaduni wa kutoa kauli zinazofuata haki za binadamu na kuheshimu utawala wa kisheria

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi mtendaji wa kituo hicho, Dk Hellen Kijo Bisimba  kuwa hivi karibuni kumekuwa na matamshi yenye kuwatia hofu wananchi yanayotoka kwa wanasiasa na vyombo vya dola kuleta sintofahamu kwa wananchi.

“Kumekuwa na hali ya kutishiana baina ya viongozi wa vyama, viongozi wa serikali hususani mawaziri, jeshi la polisi, kauli za kuleta hofu kwa wananchi kwa kauli ambazo Watanzania hawana uzoefu nazo kama maneno haya, mfano wa maneno dikteta uchwara, ukuta, tutawashughulikia,viberiti vya gesi, sijaribiwi”, alisema Dk Hellen.

Pia amelitaka jeshi la polisi liache kuzuia mikutano ya nje na ndani ya vyama vya siasa na kuwazuia wanasiasa kwenda watakako kwani huko ni kuingilia uhuru na hususan uhuru ambao umeanishwa katika ibara ya 17 ya katiba ya Jamhuri ya Muungano

Raia Wazidi Kuondolewa Katika Mji Wa Darayya Nchini Syria
Trump Asisitiza Kujenga Ukuta Kuwazuia Wahamiaji