Kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM (NEC) kinachoendelea kufanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam chini ya Mwenyekiti wa chama hicho, Dkt. John Pombe Magufuli kimewapitisha wajumbe wapya wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa na NEC.

Wajumbe hao ni Waziri Mkuu Mstaafu wa awamu ya nne, Mizengo Peter Pinda pamoja na Makongoro Nyerere.

Kikao hicho pia kimepiga kura ya kuwapata wajumbe sita kwa kuzingatia jinsia, watatu kutoka Tanzania Bara na watatu kutoka Tanzania Zanzibar ambao watakuwa wajumbe wa Kamati Kuu.

Jumla ya majina 18, tisa kutoka kila upande yalipendekezwa kuwania nafasi hizo.

Waziri Mkuu Mstaafu wa awamu ya nne Mh. Mizengo Pinda na Makongoro Nyerere waliteuliwa na  Rais Dkt. Magufuli  hivi karibuni kabla siku ya leo Mei 28, 2018 kupitishwa rasmi.

Urusi 2018: Nani atabeba Kombe? Tuimulike Argentina
Jamie Maclaren aitwa kuchukua nafasi ya Tomi Juric