Mshambuliaji na nahodha wa mabingwa wa soka barani Ulaya (Timu Ya Taifa Ya Ureno) Cristiano Ronaldo, ni miongoni mwa wachezaji walioorodheshwa kwenye kikosi bora cha michuano ya Euro 2016, iliyofikia tamati mwishoni mwa juma lililopita huko nchini Ufaransa.

Kikosi bora cha michuano hiyo kimetajwa mapema hii leo na shirikisho la soka barani Ulaya UEFA.

Ronaldo aliwahi kujumuishwa katika kikosi cha Euro 2004 sambamba na 2012.

Raia mwenzake anaecheza katika nafasi ya ulinzi Pepe, naye ametajwa katika kikosi hicho na aliwahi pia kujumuishwa mwaka 2008 na 2012.

Miaka ya nyuma UEFA walikua wakitaja kikosi cha wachezaji 23 waliofanya vyema katika fainali za Euro, lakini kwa mwaka huu orodha hiyo imepunguzwa na kufikia idadi ya wachezaji 11.

Kikosi hicho kimeteuliwa na kamati ya ufundi ya shirikisho al soka barani Ulaya UEFA na miongoni mwa wajumbe yupo Sir Alex Ferguson na David Moyes ambao wote waliwahi kuwa wakuu wa benchi la Man Utd.

“Tunaamini kikosi hiki kinawakilisha wachezaji bora zaidi walioshiriki michuano ya Euro 2016,” Amesema, Ferguson, ambaye ni balozi mwema wa ukufunzi wa UEFA.

Kikosi cha wachezaji 23 kilichotajwa na kamati hiyo ya ufundi yupo mlinda mlango Rui Patrício (Ureno)

Mabeki: Joshua Kimmich (Ujerumani), Jérôme Boateng (Ujerumani), Pepe (Ureno) na Raphaël Guerreiro (Ureno)

Viungo: Toni Kroos (Ujerumani), Joe Allen (Wales); Aaron Ramsey (Wales) na Dimitri Payet (Ufaransa).

Washambuliaji: Antoine Griezmann (Ufaransa) na Cristiano Ronaldo (Ureno)

Lil Wayne aandamwa na Kifafa, alazwa ICU
Tailor Swift afunika mastaa walioingiza pesa nyingi zaidi, Jackie Chain naye yumo