Kikosi cha mabingwa wa zamani wa Afrika, Al Ahly ya Misri kinatarajiwa kuwasili kesho Dar es Salaam, tayari kwa mchezo wa mkondo wa kwanza wa ligi ya mabingwa barani Afrika dhidi ya Young Africans utakaochezwa siku ya Jumamosi.

Kikosi cha Al Ahly kinachonolewa na kocha kutoka nchini Uholanzi Martin Jol, kitawasili na ndege maalum ya kukodi tayari kwa mchezo huo utakaopigwa kwenye uwanja wa taifa jijini Dar es salaam.

Ahly inatarajiwa kufikia katika hoteli ya Serena, Dar es Salaam na itakuwa ikifanya mazoezi kwenye Uwanja wa Gymkhana Club hadi Ijumaa itakapohamia Uwanja wa Taifa.

Na kikosi kinachotarajiwa kutua kesho ni makipa; Ahmed Abdul Monem, Mosaad Awad, Sherif Ekramy.

Mabeki; Ahmed Fathy, Bassem Ali, Mohamed Hany, Rami Rabia, Saad Samir, Ahmed Hagazy na Sabri Rahil.
Viungo; Amir El-Sulaya, Ahmed El El- Sheikh, Walid Soliman, Abdalla El Said, Hossam Ghaly, Hossam Ashour, Ramadan Sobhi na Momen Zakaria.
Washambuliaji; Malick Evouna, Emad Moteab na Amr Gamal.

Mahakama ya ICC yafuta kesi dhidi ya makamu wa rais wa Kenya na Mwandishi
Serikali yakanusha kunyimwa misaada na nchi za Magharibi