Wachezaji Andreas Pereira (Manchester United) na Artur (FC Barcelona) ni miongoni mwa walioitwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Brazil, kitakachocheza michezo ya kimataifa ya kirafiki mapema mwezi ujao dhidi ya Marekani (USA) na El Salvador.

Pereira mwenye umri wa miaka 22 ambaye msimu uliopita alicheza kwa mkopo Valencia CF ya Hispania akitokea Manchester United, amewashtua wengi baada ya kutajwa kwenye kikosi cha kocha Tite.

Artur ambaye aliitwa kwenye kikosi cha maandalizi ya kombe la dunia na baadae kutemwa, anapewa nafasi kubwa ya kumshawishi kocha huyo, na huenda akapata nafasi ya kudumu katika kikosi cha kwanza.

Wachezaji walioachwa katika kikosi cha Brazil kitakachocheza michezo hiyo miwiwli ya kimataifa ya kirafiki ni beki wa kushoto wa klabu bingwa barani Ulaya Real Madrid Marcelo, Miranda wa Inter Milan, kiungo wa Guangzhou Evergrande Paulinho pamoja na Fernandinho na Gabriel Jesus wa Manchester City .

Mlinda mlango wa Manchester City Ederson ameachwa kutokana na sababu binafsi, na nafasi yake imechukuliwa na kipa wa klabu ya Flamengo Hugo.

Brazil wataanza kucheza na Marekani mjini New Jersey Septemba 07 na siku nne baadae watapambana na El Salvador mjini Washington.

Kikosi kamili kilichotajwa kwa ajili ya michezo hiyo ya kimataifa ya kirafiki upande wa Makipa: Alisson (Liverpool), Hugo (Flamengo) na Neto (Valencia)

Mabeki: Alex Sandro (Juventus), Dede (Cruzeiro), Fabinho (Liverpool), Fagner (Corinthians), Felipe (Porto), Filipe Luis (Atletico Madrid), Marquinhos (Paris St Germain) na Thiago Silva (PSG)

Viungo: Andreas Pereira (Manchester United), Arthur,(Barcelona), Casemiro (Real Madrid), Fred (Manchester United), Lucas Paqueta (Flamengo), Phillipe Coutinho (Barcelona) na Renato Augusto (Beijing Guoan)

Washambuliaji: Douglas Costa (Juventus), Roberto Firmino (Liverpool), Neymar (PSG), Pedro (Fluminense) na Willian (Chelsea) na Everton (Gremio).

Ngome ya Mbowe yazidi kumong'onyoka
Madiwani waonywa kujihusisha na biashara