Kiungo wa Man Utd, Bastian Schweinsteiger ametajwa katika kikosi cha timu ya taifa ya Ujerumani ambacho kitaingia kambini kujiandaa na michuano ya Euro 2016.

Kiungo huyo ametajwa kwenye kikosi cha Joachim Low, kilichosheheni wachezaji 27, na kuibua maswali mengi kwa wadau wa soka duniani kufuatia majeraha yanayomkabili kwa sasa.

Hata hivyo kikosi kilichotajwa hii leo, kitapunguzwa na kufikia wachezaji 23, ambacho kitashiriki fainali za Euro 2016, hivyo inaaminiwa huenda Schweinsteiger akaondolewa, kama hatofikia kiwango.

Schweinsteiger, amekua nje kwa kipindi kirefu bila kujumuishwa kwenye kikosi cha Man Utd ambacho hii leo kitamalizia mchezo wa mwisho wa ligi kuu ya soka nchini England.

Kikosi kamili cha Ujerumani kilichotajwa hii leo, upande wa makipa yupo Neuer, Leno, ter-Stegen

Mabeki: Mustafi, Hector, Howedes, Hummels, Can, Rudiger, Boateng, Rudy

Viungo/Washambuliaji: Khedira, Schweinsteiger, Ozil, Schurrle, Podolski, Reus, Muller, Draxler, Kroos, Gotze, Bellarabi, Gomez, Brandt, Sane, Weigl, Kimmich.

Kabla ya kuelekea nchini Ufaransa tayari kwa Euro 2016, kikosi cha timu ya taifa ya Ujerumani kitacheza mchezo miwili ya kimataifa ya kirafiki dhidi ya Slovakia mnamo Mei 29 na kisha dhidi ya Hungary, Juni 04.

Michezo ya Ujerumani katika fainali za Euro 2016 itaanzia June 12: (Ujerumani vs Ukraine) June 16: (Ujerumani vs Poland) na  June 21: (Ireland Ya Kaskazini vs Ujerumani).

Mabingwa Watetezi Nao Wataja Kikosi, Manguli Waachwa
Kikosi Cha Serengeti Boys Chatakata Mbele Ya Wenyeji

Comments

comments