Kikosi cha vinara wa ligi kuu soka Tanzania Bara Simba, kimeanza safari asubuhi ya leo kutoka mkoani Iringa kuelekea mkoani Njombe, kwaajili ya mchezo wake wa ligi kuu dhidi ya Njombe Mji.

Kikosi cha Simba kiliondoka jijini Dar es salaam Ijumaa iliyopita na kutua Mkoani Iringa ambako kiliweka kambi ya muda ambapo jana kilifanya mazoezi katika uwanja wa Samora mkoani humo.

Mchezo huo wa raundi ya 21 kwa Simba na 22 kwa Njombe Mji utapigwa kesho April 3 kwenye uwanja wa Sabasaba mjini Njombe kuanzia saa 10:00 jioni.

Simba kwasasa ipo kileleni ikiwa na alama 46 sawa na Yanga yenye alama 46 zikitofautiana idadi ya mabao ya kufunga na kufungwa. Njombe Mji ipo nafasi ya 15 ikiwa na alama 21 katika michezo 18.

 

Chombo cha Anga za Juu cha China chaanguka
Video: DataVision International yatoa msaada kwa kituo cha watoto yatima

Comments

comments