Kikosi cha Simba SC leo Ijumaa (Septemba 23) kinaelekea Kisiwani Unguja (Zanzibar), kwa ajili ya Michezo miwili ya Kirafiki katika kipindi hiki cha kupicha Michezo ya Kimataifa iliyo kwenye Kalenda ya Shirikisho la Soka Duniani ‘FIFA’.

Simba SC inayoshiriki Ligi Kuu Tanzania Bara na Ligi ya Mabingwa Barani Afrika msimu huu 2022/23, inaelekea kisiwani humo, kufuatia Mwaliko wa Shirikisho la Soka visiwani Zanzibar ‘ZFF’ ambalo limeandaa michezo ya kirafiki itakayopigwa Uwanja wa Aaman.

Meneja Habari na Mawasilino wa Simba SC Ahmed Ally amesema wanakwenda kucheza na Kipanga FC inayoshiriki Ligi Kuu ya Zanzibar na Kombe la Shirikisho Barani Afrika, kisha watakipiga na Malindi FC.
Amesema Mchezo wa kwanza watacheza keshokutwa Jumapili (Septemba 25) dhidi ya Kipanga FC, kisha Jumanne (Septemba 27) watapapatuana na Malindi FC.

“Michezo hii itatuweka sawa na kuwafanya wachezaji wetu kuendelea kuwa na utimamu wa mwili katika kipindi hiki ambacho ligi zimesimama kupisha kalenda ya FIFA, tunaamini Benchi letu la Ufundi chini ya Kocha Mgunda litawatumia wachezaji waliobaki kikosini ili kuwajenga kikamilifu kabla ya kuendelea na Ligi Kuu na Ligi ya Mabingwa mapema mwezi Oktoba.”

“Tukimaliza kucheza michezo hii miwili kikosi chetu kitarejea Dar es salaam Septemba 28, kwa ajili ya kuendele na Program nyingine za maandalizi ya kuikabili De Agosto ya Angola.” amesema Ahmed Ally

Simba SC itaanzia ugenini nchini Angola kucheza dhidi ya De Agosto Oktoba 08, kisha itamalizia nyumbani Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam, Oktoba 15.

Tanzania Prisons: Tupo vizuri, tunawasubiri Azam FC
Wagomea chanjo ya surua, Watoto 700 wafariki