Kikosi Maalum cha Operesheni kutoka Makao Makuu ya Jeshi la Polisi nchini kimewasili mkoa wa Njombe chini ya kamishna wa operesheni na mafunzo wa jeshi hilo, Nsato Marijani.

Akizungumza mkoani humo, Marijani amewataka wananchi kutoa ushirikiano ili kuweza kuwabaini watu wanaofanya vitendo ya utekaji na mauaji dhidi ya watoto wadogo.

‘’Mimi sio mtu wa maneno mengi sana ila naamini sisi wote hapa tukishirikiana hawezi mtu akajificha, mtu ataweza kujificha kama hamtatoa ushirikiano, kutoa taarifa, sasa mimi nitazipata taarifa kwa hiyari au kwa shari ntazipata tu’’amesema Marijani.

Aidha, Marijani amesisitiza ushirikiano kabla ya kuanza kuchukua hatua kali dhidi ya wale ambao wamekuwa wakipoteza maisha ya Watanzania wasiokuwa na hatia halafu wao wakabaki wakiendelea na maisha yao.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Christopher Ole Sendeka amesema kuwa kufuatia kuwasili kwa kikosi hicho wanaofanya mauaji ya watoto wadogo hawatakuwa na nafasi ya kukatisha katika ardhi ya Njombe.

Hata hivyo, Ole Sendeka ametoa wito kwa wananchi mkoani Njombe kuwafichua watu wanaotajwa katika makundi matatu yanayojihusisha na matukio ya mauaji wakiwemo wafanyabiashara

Video: Ukifika muda wako utumie, mtajuta - Manara
Video: Masanja amuomba Makonda kuwanasua wasanii kwenye upangaji