Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa Awamu ya Nne, Jakaya Mrisho Kikwete amevunja ukimya na kutoa neno la kumkaribisha aliyekuwa mjumbe wa kamati kuu ya Chadema, Edward Lowassa kujiunga tena na chama chake cha zamani CCM.

Kwenye Ukurasa wake wa Twitter, Rais Mstaafu wa awamu ya nne, Jakaya Kikwete ameandika ujumbe wa kumkaribisha Lowassa, huku akitoa pongezi kubwa kwake kwa kurudi nyumbani kwaajili ya kuendelea kukiimarisha chama.

Hata hivyo baada ya Kikwete kuandika ujumbe huo katika mtandao wake wa kijamii, Mbunge wa Nzega Mjini kupitia chama cha mapinduzi (CCM), Hussein Bashe, amemjibu kwa kuandika ujumbe akimlaumu Kikwete kuwa Lowassa aliondoka CCM kwa sababu yake.

Kangi Lugola aliliwa Kondoa, 'Baba tusaidie na hawa polisi'
Habari kubwa katika magazeti ya Tanzania leo Machi 2, 2019

Comments

comments