Mbunge wa jimbo la Chalinze wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani, Ridhiwani Kikwete ameipongeza Benki ya NMB kwa juhudi zao za kutoa misaada kwa jamii ili kutatua changamoto mbalimbali zinazokuwa zikiwakabili wanajamii.

Akitoa pongezi hizo jana, katika kata ya kiwangwa alipokuwa akipokea vifaa mbalimbali vya hospital vilivyotolewa na benki hiyo, Ridhiwani amesema kuwa awali hospitali hiyo ilikuwa na changamoto ya vitanda kwa ajili ya kinamama kuweza kujifungua lakini kutokana na msaada huo tatizo hilo limebaki kuwa ni historia .

“Naipongeza benki ya NMB kwa kutambua thamani ya kinamama wa Chalinze ingawa katika nchi yetu kuna changamoto nyingi sehemu zingine lakini nyie mmeamua kutuletea misaada huu katika halmashauli yetu ya chalinze”Alisema Ridhiwani

“Mimi nawatia moyo tu kwa niaba ya wananchi wa Chalinze msichoke kutusaidia kwani mahitaji yetu bado ni mengi ingawa nasi kama serikali tunapambana ili kuihakikisha kinamama wanajifungua bila matatizo ya aina yeyote hile ndio maana hata vifo vya kinamama chalinze wakiwa wanajifungua vinazidi kubaki kuwa historia”

Aliongeza kuwa awali walikuwa wanakabiliwa na tatizo la ukosefu wa viwanda kwa ajili ya kinamama kujifungulia katika hospital hiyo lakini Nmb imewapatia vitanda 10 kwa ajili ya kupunguza tatizo hilo hivyo amewataka wananchi wa kata hiyo kwa kushirikiana na watumishi wa hospital hiyo kuhakikisha wanavilinda vifaa hivyo ili viweze kuwasaidia kwa kipindi kirefu.

Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Halmashauli ya Chalinze, Dr Rahim Hangai amesema kuwa kipindi cha nyuma kinamama walikuwa wanapoteza maisha yao wakati wa kujifungua kutokana na changamoto mbalimbali kwa sasa ni wastani ya mama mmoja kupoteza maisha kila mwaka kwa watu laki moja wakati wa kujifungua hii ni hatua kubwa sana katika halmashauli yetu ya chalinze.Alisema.

Aidha Dr Hangai alisema kuwa vifaa hivyo vimekuja kwa muda mwafaka kutokana maombi yetu ilikuwa ni kupata vifaa na Nmb wametuletea hivyo chalinze itabaki ni historia vifo vinavyotokana na uzazi kwa kinamama.

“Napenda kuwaomba watumishi wa idara ya afya katika halmshsuli ya chalinze kila mmoja kwa nafasi yake kuhakikisha anapambana ili kuwasaidia wagonjwa wanaokuja kupata huduma ili chalinze iendelee kuongoza kwa utoaji wa huduma za kiafya hapa nchini”Alisema De Hangai.

Naye Meneja wa Benk ya NMB Wilaya ya Bagamoyo Bi, Bertha Mungure alisema kuwa benk hiyo imetoa msaada wa vifaa mbalimbali katika jimbo la chalinze na vyenye thamani ya shilingi ya milioni kumi ka lengo la kutoa faida wanazozipata kwa jamii ili kuisaidia serikali baadhi ya changamoto zinazokuwa zikiwakabili wananchi.

Aliongeza kuwa benk hiyo itaendelea na kutoa misaada mbalimbali kwa kipindi chote kwani kwa kipindi hiki benk imetenga fedha nyingi za kusaidia katika jamii ili kuweza kulipa fadhila kwa wateja wake.

“Vifaa vilivyotolewa ni vitanda vya kujifungulia 10,vitanda vya kawaida 6,magodoro10,delvery kit 1na Bm Mashine 6 vyote vikiwa na thani ya milioni 10”Alisema Meneja huyo

Aidha amempongeza mbunge wa jimbo hilo kwa ushirikiano anaonyesha katika benk hiyo kwa kuwasisitiza wananchi wake kufungua akaunti katika benk ya Nmb na kuachana na tabia ya kukaa na pesa ndani ya nyumba huku mahali pa kuzihifadhi ipo.

Maajabu mapacha kuolewa na mwanaume mmoja
Sumaye: Dkt Bashiru ajiandae kuchukiwa CCM