Rais mstaafu wa Awamu ya Nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amesema kuwa amesikitishwa na taarifa za uzushi zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii za kumhusu yeye akionekana kujibu moja ya kauli ya Rais wa sasa Dkt. John Pombe Magufuli kitu ambacho si kweli.

Kikwete ametumia mtandao wake wa twitter kuonyesha masikitiko yake hayo kwa watu wanaofanya jambo hilo huku akionyesha kusikitishwa zaidi na mapokeo ya watu ambao wengi wao wameamini hiyo kauli wakidhani huenda ni kweli imetoka kwake kitu ambacho si cha kweli

“Nasikitishwa sana na uvumi huu unaosambazwa juu yangu. Inasikitisha sana. Inasikitisha zaidi kuwa wako watu timamu wanaoamini uzushi huu,”ameandika rais mstaafu Jakaya Kikwete kwenye ukurasa wake wa twitter 

Hata hivyo, hii si mara ya kwanza kwa kiongozi huyo mstaafu kuzushiwa uzushi na watu kupitia katika mitandao ya kijamii ambapo mara kwa mara amekuwa akiwasihi wanaofanya hivyo kuacha mara moja

Naibu waziri Anastazia Wambura aitaka TFF kushirikiana na serikali kuleta maendeleo ya soka
Kichanga chaokotwa na ujumbe mzito