Rais mstaafu wa awamu ya Nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amewataka wamiliki wa viwanda vya matunda kuacha kuwakandamiza wakulima kwa kununua matunda kwa bei ya chini .

Dkt. Kikwete ambae pia ni mkulima wa Mananasi amesema kuwa viwanda hivyo vinasaidia kupatikana kwa masoko ya ndani lakini vimekuwa havina uwiano wa gharama zinazolingana na maumivu anayoyapata mkulima.

Amesema kuwa kumekuwa na changamoto ya kushuka kwa soko kwa wakati mwingine hali inayokuwa ikisababisha wakulima kupata hasara kwa matunda kuoza yakiwa mashambani .

Dkt. Kikwete amesema hayo wakati Mwenge wa Uhuru ulipokwenda kutembelea shamba lake, ambapo ametoa taarifa za shamba hilo la Mananasi lililopo wilayani Bagamoyo.

Amesema viwanda vya usindikaji matunda mbalimbali, vinapaswa kumjali mkulima ambaye amekuwa akipata shida na kutumia gharama kubwa kuandaa shamba .

“Wakati utafika watakosa matunda ,kutokana na gharama yao hailipi ,wakulima wa matunda tushindwa kukubali kuuza kwa bei ya chini ambayo hailipi ” alifafanua .

Dkt. Kikwete amesema, shamba lake lina ukubwa wa hekari 200 ambapo hekar 64 ndizo zimelimwa na zipo kwenye hatua ya palizi .

“Mwenge kuangaza shambani kwangu ni ishara ya nuru, basi nitapata neema baadae, nashukuru kwa kuja kutembelea shamba langu kujionea shughuli nazofanya baada ya kustaafu” amesema Dkt. Kikwete

Video: Rungwe azungumzia uteuzi wa Anna Mghwira, aeleza maamuzi yake kama akipata uteuzi
Video: Sh. Bilioni 53.9 zaokolewa, ni kutokana na vita dhidi ya rushwa