Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Rais Mstaafu Jakaya Kikwete, amekagua hosteli za wanafunzi zilizotumika kama karantini kwaajili ya kuanza kutumika Juni 01, 2020 baada vyuo kutangazwa kufunguliwa rasmi ambapo amsema zipo tayari kwa matumizi.

Amesema kuwa hosteli hizo zipo salama na zimefanyiwa usafi wa kutosha baada ya kuondoka waliokuwa wamehifadhiwa karantini.

“Nilivyosikia wanasema wanawaleta hapa hosteli hao wageni ambao wanatoka nje ya nchi kwaajili ya karantini shaka yangu ilikuwa itakuwaje kama hawa watu watakuwa na maradhi je hawataacha mbegu kwa watoto wetu kupata huo ugonjwa” amesema Kikwete.

Amuuza mwanae baada ya kufukuzwa nyumbani

“Kabla ya kuruhusu tulijiridhisha, hatutaki hii kambi ionekane ni ‘Center’ ya kuambukiza magonjwa. Wasije kusema unaona serikali imeleta watu na kuwaachia ugonjwa,” Amesema kikwete

Boti za Zanzibar I, II zasitisha safari baada ya kupata hasara

“Tulikuwa na hofu kama ugonjwa utaendelea hadi Oktoba ingekuwa ni shida kwetu kwani kuna wanafunzi walitakiwa kumaliza chuo Mei na wengine Oktoba hapa ingetulazimu kusogeza mbele,” Ameongeza Kikwete.

Aidha amebanisha kuwa maandalizi yako vizuri na tayari wanafunzi wamejisajili kwa ajili ya masomo.

Watumiaji wa Instagram kuanza kunufaika na IGTV
Ndalichako: Marufuku wanafunzi kwenda shule na Tangawizi, malimao, na spriti