Mwenyekiti wa CCM Taifa, Jakaya Kikwete amesema kuwa mgombea urais wa chama chake, Dkt. John Magufuli tayari ameshashinda katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu na anasubiri kuapishwa.

Akiongea leo kwenye mkutano wa kufunga kampeni za chama hicho zilizofana na kuhudhuriwa na maelfu ya wananchi jijini Mwanza, alisema kuwa kutokana na jinsi ambavyo maelfu ya watu wanamuunga mkono mgombea huyo tayari ameshashinda katika kinyanyiro hicho.

Aidha, Kikwete alieleza kuwa mgombea huyo ana sifa za kuwa rais hususan katika mkakati wake wa kupambana na ufisadi na kuukemea bila woga huku akimtofautisha na mshindani wake mkubwa, Edward Lowassa wa Chadema.

Alisema kuwa Dkt. Magufuli ni mwaminifu kwa kuwa amefanya kazi kwenye wizara ya ujenzi yenye ushawishi mkubwa wa fedha, pamoja na wizara ya ardhi lakini hakuwahi kuhusishwa na kashfa yoyote.

Katika hatua nyingine, Kikweke aliisifia hali ya afya ya mgombea wa chama hicho huku akiikejeli hali ya afya ya mshindani wake mkubwa na kwamba kigezo cha afya kilitumika katika kumpaga mgombea wa chaama hicho.

Aliwataka wananchi kumchagua Dkt. Magufuli akimnadi kuwa ndiye atakayewaletea maendeleo ya kweli.

 

Kingunge Atoa Maneno Mazito Kwa CCM Na Kikwete
Kesi Ya Mita 200 Kukatiwa Rufaa